Friday, October 21, 2016

MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE MHE.JOSEPHAT MAGANGA ATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI PAMOJA NA WARATIBU ELIMU KATA.





Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga ametoa semina elekezi kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na waratibu elimu kata juu ya maadili ya kazi ya Ualimu na namna ya kusimamia Sheria na kanuni za elimu .

Kwasababu kumekuwepo na tuhuma ya wanafunzi wa kike kuwa na mauhusiano na walimu shuleni hadi kupelekea wanafunzi hao kupata ujauzito na wahusika baadhi yao ni walimu kujaribu kutoa ujauzito huo ili kupoteza ushahidi hali ambayo imesababisha wanafunzi kupoteza maisha yao na wengine kunusurika kifo, wengine kuacha shule kabisa, na taarifa hizi zimekuwa zikifichwa kwanzia ngazi ya kijiji,kata na mashuleni kutokana na  wazazi, walezi na baadhi ya walimu kusaidiana kuficha taarifa hizi .

Aidha hali hii inayoonekana kukithiri umuhimu wa semina elekezi kwa walimu ambao pengine wamesahau au hawazijui sheria na kanuni hizo ndiyo maana nimeambatana na wanasheria kutoka taasisi za umma zilizopo wilayani hapa ili kutoa ufafanuzi wa sheria hizi jinsi zinavyofanya kazi .
Mkuu wa Wilaya mhe.Josephat Maganga ameelekeza wakuu wa shule kushirikiana na bodi ya shule kuandika taarifa ya matukio ya ujauzito yanayotokea katika shule zao na kuhakikisha zinafika ofisi ya afisa elimu wilaya ambapo ataipeleka ofisi ya Mkuu wa wilaya, pia walimu wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ya Ualimu, “bahati nzuri nilishawahi kuwa mwalimu katika chuo cha Ualimu, nikapanda ngazi na kuwa afisa elimu Wilaya Serengeti, Biharamulo na Chato, kutokana na kufanya kazi kwa kusimamia kanuni na sheria nikapanda na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, na sasa ni Mkuu wa Wilaya hakika nitaendelea kusimamia na kutekeleza kanuni na sheria “alisema Maganga.

Alisisitiza kila mwalimu anawajibu wa kuhakikisha mwanafunzi anayeanza shule anasimamiwa vizuri mpaka anamaliza shule na walimu kuacha kukaa kimya wanapopata matatizo.

 Baada ya semina elekezi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mhe. Josephat Maganga ameagiza wakuu wa shule, waratibu elimu kata kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi, pili walimu kuhakikisha wana kanuni na sheria, tatu daftari la adhabu shuleni, mwisho wanafunzi wa kike kuchunguzwa ujauzito kila baada ya miezi mitatu (3) na Maafisa elimu wilaya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.


Tusa D Mwambenja
Afisa Habari na Uhusiano
BUKOMBE.

21/10/2016

No comments:

Post a Comment