Tuesday, October 18, 2016

Bukombe yaadhimisha siku ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya usafi katika Soko kuu na Stendi kubwa ya Mabasi Wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Josephat Maganga na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Bukombe washiriki katika maadhimisho ya siku ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya usafi soko kuu la Ushirombo na stendi kubwa ya mabasi  huku wafanya biashara,watumishi wa taasisi za umma wilayani na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wakishiriki kikamilifu katika zoezi la usafi.


Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Ndugu Dionis Myinga wakizoa taka na kutupa kwenye gari la kuzolea taka kwaajili ya kwenda kutupwa Dampo.



 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya ulinzi na usalama wakijadili jambo baada ya kuzungukia maeneo ya biashara sokoni na stendi ya mabasi na kujionea hali ya usafi wa maeneo hayo.
 Kamanda wa TAKUKURU wilayani Bukombe Ndg.Chuzela Shija akikusanya taka ili ziweze kuzolewa na kupelekwa mahali husika.

 Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (CWT) Wilaya Bi.Twaiba naye alishiriki zoezi hilo kikamilifu.
 Wafanyabiashara wa soko la ushirombo wakishiriki kikamilifu kuadhimisha siku ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya usafi katika soko lao.
 Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katente Bi.Annastera Kiyo akishirikiana na mwananchi wake kuhakikisha solo linakuwa safi na salama kwa wananchi.
Afisa Tawala wilayani Bukombe Ndugu Ally Mketo pamoja na vijana wa mii wa ushirombo wahakikisha vikaratasi vidogo vidogo vinatoweka kabisa maeneo hayo.

Afisa Mazingira wa Wilaya Ndugu Innocent Kailembo akihamasisha vijana ambao ni wafanya biashara wadogowadogo kuhakikisha mazingira yao ya biashara ni sari ili kulinda afya zao na afya za wateja wao.

 Skauti wafanya usafi katika meza za wafanyabiashara soko la Ushirombo ili wamiliki wa meza watakapokuja kufanya biashara wajifunze na waone umuhimu wa kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe atoa rai kwa Mwananchi wa Bukombe kujenga tabia ya kufanya usafi kila siku katika maeneo yao ya shughuli mbalimbali na makazi ili kuepuka magonjwa ya Mlipuko " Wananchi wamehamasika na kushiriki zoezi hili kikamilifu sasa lisiwe la leo bali liwe endelevu kwa kujenga tabia ya kufanya usafi maeneo ya shughuli mbalimbali na makazi kuepuka milipuko ya magonjwa " alisema Maganga Mkuu wa Wilaya.

No comments:

Post a Comment