Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bukombe Ndugu Dionis M. Myinga Anapenda
Kuwataarifu Wananchi wote wa Wilaya ya
Bukombe kuwa tarehe 07/09/2016 hadi
tarehe 08/09/2016.
Jumla ya Wanatahiniwa 3975 watafanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Wasichana wakiwa
2062 na Wavulana 1913. Shule za Serikali 75 na shule ya Binafsi 1 Jumla ya Shule 76 kwa Mwaka huu zinatarajiwa kufanya Mitihani ya darasa la Saba
Wilayani Bukombe.
Hivyo Ukiwa Kama Mzazi, Mlezi na Jamii ya Bukombe ni
Jukumu Letu kuwaombea Wanafunzi wetu wa Darasa la Saba Mtihani Mwema Mungu
akawaongoze kufanya Vyema.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
Anasisitiza watahiniwa kufuata taratibu zote watakazoelekezwa na wasimamizi na
kuwa watulivu kipindi chote cha kufanya Mitihani yao ya kumaliza Elimu ya
Msingi
Nawatakia
kila kheri.
Imetolewa na;
Tusa D Mwambenja
Afisa Habari
BUKOMBE.
No comments:
Post a Comment