Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga awaomba wajumbe wa bodi mpya ya Afya kufanya kazi kwa lengo la kusaidia
wananchi katika kuimarisha Afya za jamii, kusimamia na kuendesha vizuri shughuli na rasilimali za Afya, Kuwezesha
CHMT kutimiza malengo ya bodi ya Afya.
Awaomba wajumbe wa bodi ya
Afya wasome maelekezo ya kanuni,sheria na taratibu za uendeshaji wa bodi ya
Afya na Bodi ya Afya iwe karibu na
wataalamu na wananchi wote kwa ujumla washirikiane ili kuleta maendeleo ya Afya
ya jamii. Alilisisitiza pia
Bodi ya Afya ijue na kutambua
Mazingira ya Hospital na kutoa ushauri mzuri kwa wataalamu ili kuboresha sekta Muhimu ya Afya.
Viongozi wa Dini walishuhudia uzinduzi huo wa Bodi mpya ya Afya wilayani Bukombe.
Katibu Tawala (W) Ndugu Paul Cheyo kushoto,kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya Ndugu Aubrey Moshi katika Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Afya.
Picha ya Pamoja Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Josephat Maganga ambaye alikuwa mgeni rasmi,Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe.Leokadia Kasase na Wajumbe Wapya wa Bodi Mpya ya Afya Wilayani Bukombe.
Picha ya Pamoja ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga na Wajumbe waliohudhuria Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Afya Wilayani Bukombe.
No comments:
Post a Comment