|
||||
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Bukombe Ndugu Dionis M.Myinga anapenda kuwataarifu wananchi wote wa wilaya
ya Bukombe kuwa tarehe 1/11/2016 hadi 18/11/2016 wanafunzi wa kidato cha nne
wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne.
Watahiniwa 1515 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne
wasichana wakiwa 698 wavulana 817 kutoka shule 12 za serikali na 2
binafsi na watahiniwa wa kujitegemea 107
kutoka katika vituo viwili (2)
vya watahiniwa wa kujitegemea Runzewe na Ushirombo sekondari.
Jumla ya shule 14 na vituo viwili (2)
vya watahiniwa wa kujitegemea kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanya mitihani ya
kidato cha nne wilayani Bukombe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
anasisitiza watahiniwa kufuata sheria na taratibu zote watakazoelekezwa na
wasimamizi na kuwa watulivu kipindi chote cha kufanya mitihani yao ya kumaliza
kidato cha nne .
Pia amesisitiza wasimamizi kuzingatia kanuni
na sheria za usimamizi wa mitihani zinavyoelekeza pasipo kuzivunja.
Hivyo ukiwa kama mzazi,mlezi na jamii ya
Bukombe na nje ya Bukombe ni jukumu letu kuwaombea wanafunzi wetu wa kidato cha
nne mtihani mwema na Mungu akawaongoze.
Blog yako nzuri, ukiweza kui-update mara kwa mara itakuwa nzuri zaidi. aidha hizo menu za idara mbalimbali ziwekee taarifa. kama una Website ziondowe hapa ubakize habari tu, mengine yaelekee kwenye Website
ReplyDelete