Tuesday, July 11, 2017

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 10 za Watumishi wa Afya wilayani Bukombe.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe.Benjamin Mkapa amekabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 10 za Watumishi wa Afya wilayani Bukombe zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation) katika vijiji vya Uyovu,Bulega,Bugelenga,Msasani na Miyenze.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita ikiwalisha wilaya zote za Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera  zilizopata ufadhili wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya. 
Wakati wa kukabidhi Nyumba 50 Mhe.Mkapa ametoa pongezi kwa jitihada za uboreshaji wa huduma za afya zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Mhe.Rais John Joseph Pombe Magufuli.Taasisisi ya Mkapa  itaendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za Afya kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia unaopambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukimwi, Ujenzi wa Nyumba hizo ni chachu ya uwajibikaji,uadilifu kwa watoa huduma ambao ni watumishi wa Afya, "Madaktari hakikisheni mnafanya kazi kwa kuafata taratibu za kazi na kuzingatia haki za binadamu" amesema Mhe.Mkapa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Dkt.Ellen Senkoro wakati akitoa Taarifa ya taasisi ameeleza kuwa  taasisi hiyo ni asasi isiyo ya kiserikali ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali za Mitaa na imeweza kutoa ajira takribani 1,100 kupitia Sekretarieti ya ajira,ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wasiojiweza 949, ujenzi wa Nyumba 50 za watumishi wa Afya katika Mikoa ya Geita ambapo nyumba 20 zimejengwa, 10 zimejengwa Kagera na  20 zimejengwa Simiyu na mikoa mingine ambio talari wamekabidhiwa ni katika jitihada za kuhakikisha watoa huduma wa Afya wanakaa katika Nyumba zenye mazingira mazuri ili kutoa huduma bora na kwa wakati. Bi.Senkoro ameongeza katika juhudi za kupunguza vifo vya wakina Mama wajawazito ambapo vyumba vya upasuaji (theatre) 11 katika vituo vya Afya vimejengwa.
Dkt.Senkoro amefafanua kuwa taasisi hii iliingia Mkataba wa kujenga Nyumba 480 ambapo nyumba 430 zimekamilika na nyumba 30 zinatarajiwa kukamilika mwezi Agost, kupitia mfuko huu wa Dunia(Global Fund) unaopambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukimwi,  Mikoa 17 na Halmashauri 51 zimeweza kufikiwa na vituo  vya Afya 268 vimejengwa. Katika Halmashauri ya Chato,Bukombe,Maswa, na Biharamulo ujenzi umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 wastani kila nyumba 1 ni Shilingi Milioni 35, ambapo Nyumba 22 zinatumia umeme wa kawaida na nyumba 28 zinatumia umeme wa jua. Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo ametoa shukrani kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Wizara ya Afya,Jinsia na Maendeleo,Mfuko wa Dunia pamoja na Serikali za Mitaa.
Mfuko wa Dunia unashirikiana na serial ya Tanzania tangu mwaka 2003 na mwaka  huu 2017 mfuko umeingia mikataba 16 yenye jumla ya thamani ya shilingi Trillioni 3.8 kwaajili ya kupambana na Kifua Kikuu na Ukimwi, vigezo vya utendaji vimezingatiwa na Tanzania ni moja kati ya nchi zinazotekeleza vyema malengo ya Mfuko wa Dunia ambayo ni kuboresha huduma za afya, mwishoni mwa mwaka 2016 takribani watu laki 7 wamepatiwa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi,na katika kuendelea kupunguza maambukizi ya ukimwi condom milioni 38 zimesambazwa kupitia mfuko wa dunia. Aidha mfuko wa dunia kwa kushirikiana na serikali imejenga maghala ya kuhifadhia dawa, ufadhili wa masomo na ujenzi wa nyumba 480 kushirikiana na Mkapa Foundation pamoja na Serikali ya Tanzania. "Mfuko wa dunia unaridhishwa na Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza yote yaliyokusudiwa na Mfuko huo " amesema Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia (Global Fund) Bi. Matha Setembo.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu. 
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 10 za Watumishi wa Afya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mhe.Safari Nicas Mayala.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
Wananchi wakifuatilia Hafla ya Makabidhiano ya Nyumba 50 kwa Mikoa ya Geita,Simiyu na Kagera yaliyofanyika Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita.
Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment