Friday, April 15, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe akitembelea mradi uliopo chini ya programu ya maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEDP) awamu ya pili katika shule ya Sekondari Namonge kata ya Namonge.

Mradi huo unaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na  na Teknolojia kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Mradi unagharimu Tsh . 289,859,407 unaojumuisha Ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa,  matundu nane (8)  ya vyoo vya wanafunzi na matundu mawili (2) ya vyoo vya walimu pamoja na nyumba moja ya walimu (6 in one).


 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw. James Ihunyo  akiwa ameambatana na Mhandisi wa Ujenzi Bw.Athuman Ahungu wakikagua ujenzi wa  madarasa mawili  ambayo yamefikia hatua ya boma.
 
Ujenzi wa Nyumba moja ya Walimu (6 in one) imefikia hatua ya Boma.

Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw. Athumani Ahungu akitoa ufafanuzi wa kitaalamu juu ya maendeleo ya Ujenzi huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw. James Ihunyo aliyopo ndani ya Vyumba hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw .James Ihunyo akiwa ndani ya moja ya madarasa yanayoendelea na Ujenzi shule ya Sekondari Namonge.

1 comment:

  1. Best Casinos in Thailand: Top List & Casinos for 2021
    With an impressive list seda bet of casino games 암호화폐란 and a great 메이저 리그 분석 reputation for great bet365 우회 bonuses, you have come 위닉스사이트 to the right place. Best casino in Thailand:

    ReplyDelete