Tuesday, September 6, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Ndugu Dionis M Myinga awatakia Kila la Kheri Wanafunzi wa Darasa la Saba.






Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe  Ndugu Dionis M. Myinga Anapenda Kuwataarifu Wananchi  wote wa Wilaya ya Bukombe kuwa tarehe 07/09/2016 hadi tarehe 08/09/2016.

Jumla ya Wanatahiniwa 3975 watafanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Wasichana wakiwa 2062 na Wavulana 1913. Shule za Serikali 75 na shule ya Binafsi 1 Jumla ya Shule 76 kwa Mwaka huu zinatarajiwa kufanya Mitihani ya darasa la Saba Wilayani Bukombe.

Hivyo Ukiwa Kama Mzazi, Mlezi na Jamii ya Bukombe ni Jukumu Letu kuwaombea Wanafunzi wetu wa Darasa la Saba Mtihani Mwema Mungu akawaongoze kufanya Vyema.

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Anasisitiza watahiniwa kufuata taratibu zote watakazoelekezwa na wasimamizi na kuwa watulivu kipindi chote cha kufanya Mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi
      
Nawatakia kila kheri.


Imetolewa na;
Tusa D Mwambenja
Afisa Habari
BUKOMBE.


No comments:

Post a Comment